Wednesday, June 3, 2020

TAASISI YA RUGAMBWA GIRLS FOUNDATION YAKABIDHI VIFAA VYA KUJIKINGA NA UGONJWA WA COVID-19 (CORONA)

Leo tarehe 3 Juni, 2020 Taasisi ya Rugambwa Girls Foundation (RGF) imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti msaada wa vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa (COVID 19) unaosababishwa na virusi vya Corona vyenye thamani ya TZS. 2,000,000/= kwa Wanafunzi na Walimu wa shule ya Wasichana ya Rugambwa Sekondari iliyoko Wilaya ya Bukoba Mjini, Mkoani Kagera ikiwa ni Kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais wetu pamoja na Serikali aliyeruhusu shule kufunguliwa kwa kidato cha sita na kuungana na wazazi, walimu, walezi na wanajumuiya wa Rugambwa na wanafunzi wa  kidato cha sita  kuunga juhudi za elimu kwa mtoto wa Kike. 
Mwakilishi wa Taasisi ya Rugambwa Girls Foundation, Bi. Beatrice Van Arkadie akikabidhi msaada wa vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa COVID -19 unaosababishwa na virusi vya Corona kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti
Mwakilishi wa Rugambwa Girls Foundation, Bi. Beatrice Van Arkadie akisoma Risala
Afisa Elimu, Mkuu wa Shule, Mkurugenzi wa Mkoa, Mkuu wa Mkoa na Mwakilishi wa Rugambwa Girls Foundation, wakiwa kwenye Picha ya Pamoja
Rugambwa Girls Foundation (RGF) imesajiliwa Novemba 2015, kwa namba ya usajili  na 5216 kwa sheria Cap 318 R.E 2002.  RGF  inaundwa  na wahitimu wa Rugambwa Sekondari., hadi sasa Foundation hii ina wanachama 40 walioko katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.  Jumuiya yetu haizalishi faida (non profit organization)  Lengo kuu  la RGF  ni  kusaidia mtoto  wa kike kujitambua na kupambana na changamoto mbalimbali za elimu. Pamoja na hayo, RGF pia inajihusisha na sekta ya Afya, Mazingira na Ujasiliamali. Pamoja na kusaidia jamii kwa kutumia fedha tunazojichangisha, pia tunasaidiana wenyewe kwa wenyewe katika ugonjwa, sherehe, misiba na majanga mbalimbali, kwa kutumia miongozo tuliyojiwekea. RGF Tuna malengo ya muda mrefu na muda mfupi, ikiwamo kuanzisha Benki, kujenga mabweni, na kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum shuleni Rugambwa, na kuwapa huduma.

Miaka ya Nyuma kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi, Mkoa wa Kagera tuliweza  kufanya kampeni ya kuhamasisha wanafunzi wa Rugambwa juu ya kujitambua. Mikutano miwili ilifanyika shuleni Rugambwa na vilevile tumeweza kuwasaidia wanafunzi wasiojiweza na wenye ulemavu mbalimbali. Wenye uoni na usikivu hafifu na  wenye ualibino  kwa kuwapatia bima za afya na mahitaji kama vile madaftari, kalamu, taulo za kike na mafuta ya ngozi kazi ambayo inaendelea.  Vilevile  na tulifanya harambee kuchangisha fedha za kuweza kuinua miundo mbinu ya Rugambwa Sekondari ambapo kwa kushirikiana na TEA na wadau mbalimbali tulikusanya jumla ya Shilingi milioni 129 ambazo zimetumika kukarabati miundo mbinu hapa shuleni na kuboresha miundo mbinu ya walemavu.. Msukumo huu pia ulitoka shuleni ambapo walituomba tuweze kusaidia pale tunapoweza. Tunaamini juhudi hizi zimepelekea matokeo ya Rugambwa kuwa mazuri.


No comments:

Post a Comment