Sunday, November 17, 2019

Mwanachama wa Rugambwa Girls Foundation atoa Msaada wa Bima ya Afya

Mwanachama wa Rugambwa Girls Foundation Bi. Judith Rushanja Ndissi atoa msaada wa kumlipia Bima ya Afya ya mwaka mzima mtoto Maimuna Yahaya Mamisu mwenye ulemavu aliyeongozana na Mama yake Bi. Tunu Juma Maziku mkazi wa Tanga ili aweze kuendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Bi. Ritha Kamala akikabidhi msaada kwa Bi. Tunu Juma Maziku kwa ajili ya mwanae Maimuna (kwenye picha)

Uongozi wa Rugambwa Girls Foundation uliletewa taarifa ya uhitaji wa Bima ya afya kwa mtoto Maimuna Yahaya Mamisu kupitia kwa mwanachama mwenzetu Ritha Kamala ambaye alikutana na Bi. Tunu Juma Maziku akiwa na mwanae Maimuna wakiwa kwenye mizunguko ya kuomba msaada kwa wananchi ili wapate hela hiyo na ndipo alipoutaarifu uongozi na Mwanachama mwenzetu Judith Rushanja Ndissi alijitolea na kumlipia Maimuna, Bima ya Afya ya mwaka mzima.
Bi. Judith Rushanja Ndissi aliyetoa msaada wa Bima ya Afya ya mwaka mzima kwa mtoto Maimuna (kwenye picha)
 
Uongozi unatoa wito kwa Wanachama wote wa RGF kujitolea katika kutoa misaada kwa wahitaji.

2 comments:

  1. Asante sana Mama Ndiss kwa msaada wako. Mwenyezi Mungu akubariki sana.

    ReplyDelete
  2. Asante sana Mama Ndiss kwa msaada wako. Mwenyezi Mungu akubariki sana.

    ReplyDelete