Tuesday, July 31, 2018

Mkutano Mkuu wa Tatu (3) wa RGF uliofanyika tarehe 28 Julai, 2018 katika ukumbi wa Hotel Defrance, Sinza, Dar es Salaam


Mkutano Mkuu wa Tatu (3) wa Rugambwa Girls Foundation uliofanyika katika ukumbi wa Defrance Hotel, Sinza, Dar es Salaam, ulipitia maazimio yaliyowekwa kwenye Mkutano Mkuu wa pili (2) uliofanyika tarehe 18 Februari 2017 katika ukumbi wa Hotel Defrance, Sinza, Dar es Salaam na kujadili utekelezaji wa maaziimio hayo.

Na pia Mkutano Mkuu ulijadili zaidi jinsi ya kuinua elimu shuleni Rugambwa, na jinsi ya kupata pesa za kuweza kukarabati baadhi ya miundo mbinu ya shule, vilevile  Mkutano ulijadili jinsi ya kutafuta mahusiano na taasisi nyingine ambazo zinaweza kutoa msaada kwenye shule hiyo. 
Pia Mkutano huu umesisitiza zaidi kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum (kwa walemavu wa aina zote) na kuendelea kuwalipia Bima ya afya wanafunzi 21 ambao pia walikuwa wamelipiwa awali.
Mkutano uliwakaribisha wanachama wapya na kuchagua viongozi wapya watakao ongoza umoja huu kwa muda wa miaka mitatu ijayo.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment